Wanaharakati, Wadau na Wapenzi wote wa Kiswahili hamjambo !
Tukisherehekea “SIKU YA KISWAHILI DUNIANI ” tarehe 7 Julai, kama Kamishna wa Kiswahili wa Akademia ya Lugha ya Umoja wa Afrika (ACALAN) nchini Rwanda, nawatakia maandalizi mazuri na Siku njema ya Kiswahili Duniani.
Katika Ukuzaji na Uendelezaji wa Kiswahili ndani na nje ya Rwanda. Kwa unyenyekevu mkubwa najivunia niliyoyafanya nilipochaguliwa ikiwa ni pamoja na kushukuru na kutambua hatua iliyopigwa na Serikali ya Rwanda ya kuidhinisha Kiswahili kama Lugha rasmi ya nne baada ya Ikinyarwanda, Kiingereza na Kifaransa kama inavyoonyesha Sheria OL 20/ 02 Aprili 2017.
Ingawa bado kuna mengi ya kufanya, nimefanikiwa kwa ushirikiano mkubwa kufundisha Kiswahili kupitia Radio TV Rwanda mara tatu kwa wiki kwa muda wa miaka kumi kwa kujitolea kabisa.
Kwa kupitia mijadala mbali mbali mashuleni, vyuo na mikutano kwenye ngazi za wilaya nchini kote.
Nimefanikiwa pia kutunga na kuchapisha Vitabu vinne pamoja na Kamusi za Lugha tatu ” Kiswahili – Ikinyarwanda na Kiingereza” nikiwa na Profesa Ken Walibora, ” kutoka Kenya na” Wesomese Oluswahili n’Olungereza” nikishirikiana na James Wasula kutoka Uganda.
Vitabu vyote hivi vimeidhinishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na REB.
Nashukuru pia kwamba kwa ushirikiano na wenzangu nimeweza kutoa mchango wangu kwenye Warsha, Mikutano, Kongamano, Utafiti na Tamasha kwenye Vyuo Vikuu na Sehemu mbalimbali ndani na nje ya Afrika Mashariki hata Ulaya.
Aidha nimefanikiwa kutafsiri na kusambaza ujumbe na msamiati kuhusu UVIKO (COVID ) 19 na kuelimisha jamii kwa Kiswahili – Ikinyarwanda.
Haya yakifanyika, kwa makubaliano na Maktaba Kuu ya Umma ya Kigali , nimeanzisha ” Kiswahili Kona” ndani yake na Sasa ina zaidi ya Vitabu 500 vya Kiswahili kutoka kwa wadau na Wapenzi wa Kiswahili kutoka Afrika Mashariki.
Kazi yangu ikiwa inaendelea nashukuru sana Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki na BAKITA kwa mafunzo yao ” Kiswahili kwa Wageni” kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda ambayo nilihudhuria nikiwa na wanataaluma zaidi ya 200 mjini Kigali Juni 2023.
Ukarimu wa Ubalozi wa kunizawadia kamusi 15 za Kiswahili ulinipa nafasi ya kuzisambaza kwenye Asasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rwanda Génocide memorial, Rwanda Media Council, Association Rwandaise des Journalistes, KIgali public library KPL, n.k
Kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyosema , Nia, Sababu na Uwezo vipo ndio maana nataka kuanzisha ” RWANDA CENTER FOR KISWAHILI COMMUNICATION SKILLS” mjini Kigali kibarua ambacho ni kigumu na changamoto kubwa kifedha na Kiutendaji .
Nikiwaombeni tena nyote msaada wa aina yoyote, Ushikamano na Ushirikiano nawashukuruni kwa Usaidizi mlionipa kwa kipindi chote hiki .
Nawatakia SIKU njema ya Kiswahili Duniani.
Kwa Imani na Amani, hakika penye nia pana njia, Pamoja Twaweza.
Professor Pacifique MALONGA,
ACALAN Kiswahili Commissioner for Rwanda
